"MAISHA YANGU: KHAINI AU MUHANGA WA MAPINDUZI YA ZANZIBAR?" ni kitabu kinachoeleza historia ya Zanzibar ya hivi karibuni na vipi Muungano baina ya Zanzibar na Tanganyika ulivyoanzishwa hadi kuwepo ...
https://www.lulu.com/shop/khamis-abdulla-ameir/maisha-yangu/paperback/product-y45mm6.html
“MAISHA YANGU: KHAINI AU MUHANGA WA MAPINDUZI YA ZANZIBAR?” ni kitabu kinachoeleza historia ya Zanzibar ya hivi karibuni na vipi Muungano baina ya Zanzibar na Tanganyika ulivyoanzishwa hadi kuwepo taifa jipya la TANZANIA. Khamis Abdulla Ameir amejaribu kwa kadri ya uwezo wake kuweka sawa historia ya Muungano wa Tanzania katika njia iliokuwa sahihi kabisa, ili Watanzania wa leo na wa vizazi vijavyo, waweze kuelewa chanzo na malengo halisi ya Muungano huu.
Kitabu hiki kinasimulia historia mpya ya kileo kuhusu vipi vyama vya siasa vilivyoanzishwa Zanzibar tokea mwanzoni mwa miaka ya 1950 na vipi vyama hivyo na vyama vya wafanyakazi vilivyodai uhuru wa Zanzibar kutoka kwa Balozi Mkaazi wa Uingereza na sio kutoka kwa Mfalme Mwarabu ambaye alikuwa hana sauti mbele ya Balozi wa Uingereza. Zanzibar ilipata uhuru wake tarehe 10 Disemba, 1963 na serikali ya mseto ya ZNP/ZPPP ikakabidhiwa madaraka baada ya kushinda katika uchaguzi. Mwandishi anaeleza vipi Mapinduzi ya Zanzibar yalivyotekwa nyara na Mabeberu wa Uingereza na Marekani kwa kushirikiana na Viongozi wakuu wa Kenya, Uganda na Tanganyika ili Zanzibar isiweze kutekeleza siasa ya Kisoshalisti, ambayo nchi hiyo ilishaanza kuitekeleza kivitendo. Frank Carlucci, jasusi maarufu wa CIA, alipelekwa Zazibar na serikali yake kwa kazi moja tu, nayo ni kuizuia Zanzibar isijekuwa CUBA YA AFRIKA na kuziambukiza siasa ya Usoshalisti nchi jirani za Afrika Mashariki na Afrika kwa jumla.
Kitabu kimechapishwa na DL2A Buluu Publishing, jijini Paris, Ufaransa.
Plus de 13 millions de notices bibliographiques (imprimés, documents sonores, ressources électroniques, manuscrits, objets...) et près de 5 millions de notices d'autorité (personnes, collectivi...
French National Library Catalog Entry : FRBNF46997114
BOOK REVIEW: A Life of a Revolutionary Loyalist - The Chanzo Initiative
Khamis Abdallah Ameir, who turned 92 on May 1, 2022, is the only surviving member of the initial Zanzibar Revolutionary Council which was formed immediately after the isles' January 12, 1964 ...
https://thechanzo.com/2022/06/18/book-review-a-life-of-a-revolutionary-loyalist/
A review by Ahmed Rajab
Miraj Issa Saleh
Khamis Abdulla Ameir anasimulia hadithi ya maisha yake kwa ari na shauku kubwa - hadithi ambayo siyo ya kubuni bali ni ya kweli kabisa juu ya mambo yaliyotokea Zanzibar katika kipindi cha kilele cha Vita Baridi, COLD WAR, baina ya nchi za kibepari za Magharibi na zile za kikomunisti za Mashariki. Baada ya kueleza habari juu ya familia zake zote mbili, ambazo zilikuwa ni mitihani mitupu, Khamis anaelezea vipi aliweza kufika London, Uingereza, na kupata kazi za kutengeneza mashine za hisabu katika makampuni makubwa kadhaa ya mashine hizo.
Akiwa huko London, ndiko Khamis alipojitambulisha na kuwa muumini wa siasa za mrengo wa kushoto baada ya kukutana na akina Abdulrahman Mohammed Babu na Ali Sultan Issa na kuhudhuria mikutano na makongamano yaliyokuwa yakiandaliwa na Chama cha Kikomunisti cha Uingereza na huku akijishughulisha kuwasaidia baadhi ya viongozi wa kisiasa wa Afrika Mashariki waliokimbilia London kuendelea na harakati zao za kuzikombowa nchi zao ili zipate uhuru. Khamis aliweza kuchambuwa kwa kina kabisa siasa ya Kibepari na siasa ya Kisoshalisti na kutambuwa kuwa siasa ya Kisoshalisti pekee ndiyo mkombozi wa nchi za Afrika kwa maendeleo yao ya kisiasa, kiuchumi na kijamii.
Aliporejea Zanzibar, kabla na baada ya Mapinduzi, Khamis alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa vyama vya wafanyakazi (FPTU). Alifanya kazi kubwa ya kuviimarisha vyama hivyo kimafunzo, kimkakati na kiutendaji. Alifanya safari nyingi duniani katika nchi mbali mbali rafiki; na alitunukiwa Nishani ya Uwana Mapinduzi na Serikali ya Jamhuri ya Algeria kupitia Ubalozi wake uliopo Dar es Salaam, Tanzania.
Kitabu hiki kinasimulia historia mpya ya kileo kuhusu vipi vyama vya siasa vilivyoanzishwa Zanzibar tokea mwanzoni mwa miaka ya 1950 na vipi vyama hivyo na vyama vya wafanyakazi vilivyodai uhuru wa Zanzibar kutoka kwa Balozi Mkaazi wa Uingereza na sio kutoka kwa Mfalme Mwarabu ambaye alikuwa hana sauti mbele ya Balozi wa Uingereza. Zanzibar ilipata uhuru wake tarehe 10 Disemba, 1963 na serikali ya mseto ya ZNP/ZPPP ikakabidhiwa madaraka baada ya kushinda katika uchaguzi. Pia, Zanzibar ilikubaliwa ombi lake la kutaka uwanachama na hatimaye kupata kiti chake katika Umoja wa Mataifa (UN). Tarehe 12 Januari, 1964, chama cha ASP kiliipinduwa serikali mpya ya mseto ya ZNP/ZPPP na kutwaa madaraka. Tarehe 26 Aprili,1964, Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na ulianzishwa na hivyo kuunda taifa jipya la TANZANIA.
Matayarisho ya Mapinduzi ya Zanzibar yalifanywa kisiri na makundi matatu makubwa: Kundi la kwanza ni la Babu; Kundi la pili ni la John Okello na kundi la tatu ni la Abdalla Kassim Hanga. Msaada wa TANU na Rais Nyerere wa Tanganyika ulisaidia kufanikisha Mapinduzi hayo kwa mashirikiano yaliyotolewa na kambi ya Sukura, Tanga, Tanganyika. Vilikuwepo vile vile vikundi vidogo vidogo vya Mapinduzi vya baadhi ya wanasiasa wa ASP. Hata hivyo, kundi la Seif Bakari lililoundwa na vijana wa ASP (ASPYL) ndilo liloongoza Mapinduzi. Serikali ya ZNP/ZPPP ilikuwa dhaifu sana kutokana na makosa mengi iliyofanya kabla ya Mapinduzi na kwa hivyo haikuweza kujihami ipasavyo dhidi ya mashambulizi ya wanamapinduzi. Haya yote yanaelezwa kinaga-ubaga na Khamis ndani ya kitabu hiki.
Pia, Khamis anaeleza vipi Mapinduzi ya Zanzibar yalivyotekwa nyara na Mabeberu wa Uingereza na Marekani kwa kushirikiana na Viongozi wakuu wa Kenya, Uganda na Tanganyika ili Zanzibar isiweze kutekeleza siasa ya Kisoshalisti, ambayo nchi hiyo ilishaanza kuitekeleza kivitendo. Frank Carlucci, jasusi maarufu wa CIA, alipelekwa Zazibar na serikali yake kwa kazi moja tu, nayo ni kuizuia Zanzibar isijekuwa CUBA YA AFRIKA nakuziambukiza siasa ya Usoshalisti nchi jirani za Afrika Mashariki na Afrika kwa jumla. Matokeo ya utekaji nyara huo uliwafanya wazawa kuchukia siasa ya Usoshalisti na hasa baada ya kuiona hali mbaya yakutisha ya kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiusalama iliyotawala nchini Zanzibar baada ya Muungano. Kama Khamis anavyoeleza katika kitabu hichi, hali hii ilibuniwa na kupangwa kwa makusudi na mabeberu wa Kimarekani.
Khamis alikuwa Mjumbe katika Baraza La Mapinduzi (BLM) kwa muda wa miaka minane mfululizo. Alikuwa vile vile Mwenyekiti wa taasisi kadhaa za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ). Kwa hivyo, aliyajuwa mambo mengi yaliyokuwa yakifanywa na SMZ, mazuri na mabaya. Yote ameyaeleza kwa ufasaha mkubwa katika kitabu hiki. Pia, Khamis anaeleza jinsi Hati ya Makubaliano ya Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar ilivyoshindwa kupata ridhaa ya BLM na kusababisha Zanzibar kupoteza uhuru wake kamili wa kujiamulia mambo yake yenyewe.
Khamis alikamatwa na kutiwa jela chini ya ukatili wa Mandera (Ba Mkwe), mtesaji maarufu wa watu mahabusi. Aliishi jela kwa muda wa karibu miaka 7 baada ya kuuawa Rais Abeid Amani Karume na yeye kusukumiziwa janga la uhaini. Bila shaka ulikuwa ni mpango mkakati uliobuniwa na Mabeberu wa Kimarekani wa kuwatokomeza wale wote waliokuwa na fikra za kimaendeleo na mrengo wa kushoto ili wasiweze kushiriki tena katika siasa za Zanzibar. Lengo kuu ni kuifanya Zanzibar ibakie chini ya Utawala wa Kibeberu na hivyo kuilazimisha kuchukuwa mikopo kutoka Benki ya Dunia na IMF - taasisi ambazo zinatawaliwa na Serikali ya Marekani.
“MAISHA YANGU: KHAINI AU MUHANGA WA MAPINDUZI YA ZANZIBAR?” ni kitabu kinachoeleza historia ya Zanzibar ya hivi karibuni na vipi Muungano baina ya Zanzibar na Tanganyika ulivyoanzishwa hadi kuwepo taifa jipya la TANZANIA. Khamis amejaribu kwa kadri ya uwezo wake kuweka sawa historia ya Muungano wa Tanzania katika njia iliokuwa sahihi kabisa, ili Watanzania wa leo na wa vizazi vijavyo, waweze kuelewa chanzo na malengo halisi ya Muungano huu.
KUMBUKUMBUKU ZA ''THEORETICIAN'' KHAMIS ABDULLAH AMEIR ZIKO UWANJANI - mohamedsaidsalum
Haya ndiyo maajabu makubwa katika historia za Afrika kuwa wanaostahili kupewa sifa hawasifiwi wala hawapewi medali sifa zinakwenda kwa wale Waingereza wanawaita, ''syncopaths.'' Hawa ni wale watu ...
A critical review in Kiswahili