🇹🇿 Katika kitabu hiki, Mohammed AbdulRahman Mkufunzi anafanya tafkari ya safari ya zaidi ya miongo sita ya maisha yake, akielezea yale anayoyakumbuka, kwa kuyasikia kutoka kwa wazee, kuyaona kwa macho yake na kuyaishi tokea utotoni mwake hadi utuuzimani. Kitabu kimesheheni maelezo ya kihistoria yanayozihusu nchi tatu kuu muhimu zenye mnasaba mkubwa na mwandishi. Tanganyika, nchi aliyozaliwa, aliyokulia na kusoma masomo yake ya msingi. Zanzibar, nchi aliyotoka mama yake na baadae kuhamia kwa mintaarafu ya kukamilisha masomo yake ya sekondari. Comoro, nchi ya asili ya mababu zake, ambako baba yake mzazi aliamua kurudi na kujitosa katika harakati za kupigania uhuru wa visiwa hivyo na kupinga ubeberu.
Kupitia kitabu hiki mwandishi anawapa nafasi yao stahiki ya kihistoria na kuwaenzi wazee wake. Baba yake kwa ujasiri wake, ambae alikuwa mmoja wa waasisi wa chama cha ukombozi wa visiwa vya Comoro – MOLINACO – katika mwaka 1963. Chama ambacho kilikuwa na makao makuu yake mjini Dar-es-Salaam, na kilichokuwa kikitambuliwa rasmi na Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU). Mwandishi anampa pia nafasi yake maalum mama yake, ambae ndio chimbuko la maisha yake ya Zanzibar alikozaliwa, kwa jitihada zote alizofanya kuwalea na kuwasomesha kwa bidii na mapenzi.
Kumbukumbu hizi muhimu za maisha ya utotoni na ujanani, zina uzito sawa na zile za London, nchini Uingereza, ambako mwandishi aliishi kwa muda, na mjini Moscow, katika ule uliokuwa Muungano wa Jamhuri za Kisoshalisti za Kisovieti (USSR), ambako mwandishi alikosoma baadae, akiwa bado kijana mdogo.
Mwaka 1980 Mohammed AbdulRahman Mkufunzi alijiunga na Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Ujerumani -Deutsche Welle- akiwa mtangazaji na kustaafu katika 2019 akiwa mhariri na naibu mkuu wa Idhaa hiyo.
Kitabu hiki kifupi kina mengi yanayoacha kumbukumbu kuhusu maisha ya mwandishi na changamoto alizopitia, Miongoni mwa mambo yaliyokuwa yakimuumiza kichwa sana, ni tatizo la ubaguzi lililoibuka barani Afrika, ambalo analiita ni janga. Kwa mantiki hiyo, alipoulizwa suala la kutaka kujuwa jinsi gani anajichukulia, yeye ni nani na anatoka wapi? Jawabu yake ilikuwa fupi tu, “Mimi asili yangu ni Mngazija, ni Mtanganyika kwa kuzaliwa, Mzanzibari ikiwa ni chimbuko la mama yangu, na Mtanzania kutokana na Muungano wa mataifa mawili ya Tanganyika na Zanzibar 1964. Lakini zaidi najivunia kuwa Mwafrika."
Maisha Yangu Na Ninayoyakumbuka
Katika kitabu hiki, Mohammed AbdulRahman Mkufunzi anafanya tafkari ya safari ya zaidi ya miongo sita ya maisha yake, akielezea yale anayoyakumbuka, kwa kuyasikia kutoka kwa wazee, kuyaona kwa macho
Buy the Paperback, WorldWide
Maisha Yangu Na Ninayoyakumbuka
Katika kitabu hiki, Mohammed AbdulRahman Mkufunzi anafanya tafkari ya safari ya zaidi ya miongo sita ya maisha yake, akielezea yale anayoyakumbuka, kwa kuyasikia kutoka kwa wazee, kuyaona kwa macho
https://books.google.fr/books/about?id=ak_qEAAAQBAJ&redir_esc=y
Read freely some extracts of the book