Overblog
Editer l'article Suivre ce blog Administration + Créer mon blog

Chozi langu litafutwa lini ?
Chozi langu litafutwa lini ?

🇹🇿  Wasifu : 

Jane D. Mwanizuwa Sabini (Jane Davis).Ni mwandishi chipukizi wa simulizi riwaya na tungo za kishairi. Alizaliwa tarehe 20 Januari mnamo mwaka 1995 huko wilaya ya Uyui mkoani Tabora.

Alipata elimu ya msingi Igoko shule ya msingi na elimu ya upili Kazehill sekondari. Baada ya kupata ulemavu wa miguu na masikio akiwa kidato cha pili alihamia Kazima sekondari ambako alisoma hadi kidato cha nne.

Baada ya kuhitimu sekondari alijiunga na chuo kiitwacho Tabora Network Training college. Hapo alichukua kozi ya Ualimu wa awali ambapo alihitimu kwa ufaulu mzuri lakini hakufanikiwa kupata ajira.

Mwaka 2017 alianza rasmi uandishi wa simulizi riwaya na mashairi. Mwandishi huyu ni shujaa wa kupinga unyanyasaji wa kijinsia. Anatumia simulizi riwaya na tungo za kishairi kuelimisha na kuonya ukatili kwa wanawake, watu wenye ulemavu na ndoa za utotoni.

Maudhui :

Riwaya hii inahusu unyanyasaji wa kijinsia, ndoa za utotoni, na ukatili katika jamii ya Kiafrika. Inaelezea kwa undani namna changamoto hizi zinavyoathiri maisha ya wasichana na wanawake. Mhusika mkuu ambaye ni msichana mdogo, anakabiliana na maisha ya dhuluma, ukosefu wa haki, na shinikizo la kuolewa akiwa bado mtoto, hali inayozuia maendeleo yake ya kielimu na ndoto zake.

Katika riwaya hii, mhusika mkuu anaonyeshwa akikumbana na unyanyasaji wa kijinsia kutoka kwa wanaume wakubwa au hata watu wa karibu katika jamii, hali inayomuacha na makovu ya kimwili na kiakili. Pia, jamii inaonekana kushindwa kumsapoti, huku sheria na haki zikionekana kutotenda haki kwa wanawake na wasichana wanaokandamizwa.

Riwaya hii inabainisha changamoto wanazopitia wasichana wanaolazimishwa kuolewa wakiwa watoto, mara nyingi kutokana na umaskini au mila potofu zinazoendelezwa kizazi baada ya kizazi. Athari za ndoa hizi zinaonekana katika afya yao, elimu, na uwezo wa kujikomboa kiuchumi na kiakili.

🇫🇷 

Biographie :

Jane D. Mwanizuwa Sabini (Jane Davis) est une jeune auteure de romans et de poésie. Elle est née le 20 janvier 1995 dans le district d'Uyui, dans la région de Tabora.

Elle a effectué ses études primaires à l'école Igoko et ses études secondaires à l'établissement Kazehill. Par suite d’un handicap affectant ses jambes et son ouïe survenu en deuxième année de secondaire, elle a été transférée à l'établissement Kazima où elle a poursuivi sa scolarité jusqu'en quatrième année.

Après l'obtention de son diplôme secondaire, elle s'est inscrite au Tabora Network Training College. Elle y a suivi une formation d'enseignante préscolaire, qu'elle a achevée avec succès, sans toutefois parvenir à obtenir un emploi.

En 2017, elle s'est lancée officiellement dans l'écriture de romans et de poésie. Cette auteure est une militante engagée contre les violences sexistes. Elle utilise la narration romanesque et la poésie pour sensibiliser et dénoncer les violences faites aux femmes, aux personnes en situation de handicap et les mariages précoces.

Thématique :

Ce roman en kiswahili traite des violences sexistes, des mariages précoces et de la brutalité dans la société africaine. Il expose en profondeur la manière dont ces défis affectent la vie des jeunes filles et des femmes. Le personnage principal, une jeune fille, fait face à une existence marquée par l'oppression, le déni de justice et les pressions pour un mariage précoce, situation qui entrave son développement éducatif et ses aspirations.

Dans ce roman, le personnage principal est dépeint comme victime de violences sexistes perpétrées par des hommes plus âgés ou même des proches au sein de la communauté, la laissant avec des séquelles physiques et psychologiques. La société apparaît également défaillante dans son soutien, tandis que le système juridique et judiciaire semble incapable de rendre justice aux femmes et aux jeunes filles opprimées.

L'œuvre met en lumière les épreuves endurées par les jeunes filles contraintes au mariage précoce, souvent en raison de la pauvreté ou de traditions néfastes perpétuées de génération en génération. Les conséquences de ces mariages sont manifestes sur leur santé, leur éducation et leur capacité d'émancipation économique et intellectuelle.

Details
Publication Date
15 nov. 2024
Language
Swahili
ISBN
9781326832292
Category
Fiction
Copyright
All Rights Reserved - Standard Copyright License
Contributors
By (author): Jane Davis Mwanizuwa Sabini
Specifications
Pages
162
Binding Type
Paperback Perfect Bound
Interior Color
Black & White
Dimensions
A5 (5.83 x 8.27 in / 148 x 210 mm)
Tag(s) : #Jane Davis, #Fiction, #Riwaya, #Swahili Books, #Novel, #Human rights
Partager cet article
Pour être informé des derniers articles, inscrivez vous :