🇹🇿 Bikira Maria Mama wa Yesu Kristo ni kitabu kinachohusu historia ya Mama Bikira Maria ikianza na maandalizi ya kuzaliwa kwake; maisha yake baada ya kuzaliwa; kuchaguliwa kwake na Mungu Baba kuwa Mama wa Mkombozi kupitia ujumbe wa malaika Gabrieli; jinsi alivyomlea mwanae (Yesu Kristo) baada ya kumzaa; alivyoshiriki mateso hadi kifo cha mwanae akiwa msalabani; alivyokabidhiwa na Yesu kwa mwanafunzi aliyempenda (Yohana) kabla Yesu hajakata roho msalabani; alivyoishi na mitume wa Yesu baada ya kifo cha Yesu; kifo chake (Maria), pamoja na kupalizwa kwake mbinguni.
Pia, kinajibu maswali mengi yanayoulizwa na waumini walio ndani na nje ya kanisa Katoliki juu ya sababu za kumuomba Mama Maria atuombee kwa Mungu Baba na kwa mwanae Yesu Kristo; na juu ya ubikira wake. Majibu ya maswali hayo yanatoka kwenye Biblia Takatifu, Mapokeo Matakatifu na Mamlaka Fundishi ya Kanisa. Mwisho, kinaeleza nafasi ya Mama Maria katika imani yetu, na kina nyimbo za Mama Bikira Maria.
Mwandishi wa kitabu hiki ni mlei wa Kanisa Katoliki, Parokia ya Mt. Yakobo Mkuu Mtume, Kigango cha Tambani – Mbande, Jimbo Kuu la Dar es Salaam. Alizaliwa Mkoani Mwanza na kupata elimu yake ya msingi katika Shule ya Msingi Mkuyuni - Mwanza, mwaka 1993-1999; Shule ya Sekondari Nsumba - Mwanza, mwaka 2000-2003; Shule ya Sekondari Milambo-Tabora, akisomea mchepuo wa Lugha (Kiswahili, Kingereza & Kifaransa) mwaka 2004-2006; Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ambako alisomea shahada ya Lugha: BA Language Studies (French, Kiswahili & Linguistics) mwaka 2006-2009.
Aliwahi kufanya kazi sehemu mbalimbali kama vile: The International Languages Training Centre - Mwanza akiwa mhariri na mwalimu wa lugha; aliwahi kufundisha masomo ya lugha katika shule ya Sekondari Agape High School na Centennial Christian Seminary zilizopo Mbagala Dar es Salaam; aliwahi kuwa mhariri na mwandishi wa vitabu katika kampuni ya vitabu ya Mture Educational Publishers Limited - Mwenge, Dar es Salaam. Pia aliwahi kuwa mwandishi wa makala katika gazeti la Mwananchi. Ameandika vitabu mbalimbali vya kiada na ziada katika masomo ya lugha. Kwa sasa ni mwandishi wa vitabu wa kujitegemea.
Utume wake: aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Miito Jimbo Kuu la Tabora, katika chama cha Wanafunzi wa Katoliki Tanzania (TYCS) alipokuwa akisoma kidato cha tano na cha sita, pia amewahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi wa Jumuiya Ndogondogo.
Bikira Maria Mama wa Yesu Kristo
"Bikira Maria Mama wa Yesu Kristo" ni kitabu kinachohusu historia ya Mama Bikira Maria ikianza na maandalizi ya kuzaliwa kwake; maisha yake baada ya kuzaliwa; kuchaguliwa kwake na Mungu Baba kuwa ...
Buy the paperback, Worldwide
Bikira Maria Mama wa Yesu Kristo
🇹🇿 Bikira Maria Mama wa Yesu Kristo ni kitabu kinachohusu historia ya Mama Bikira Maria ikianza na maandalizi ya kuzaliwa kwake; maisha yake baada ya kuzaliwa; kuchaguliwa kwake na Mungu Baba...
https://books.google.fr/books/about?id=ZwlWEAAAQBAJ&redir_esc=y
Google Books, preview available everywhere in the World !